Wabunge wa viti maalum CHADEMA akiwemo Halima Mdee na wenzake leo Ijumaa wamefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuhudhuria kesi waliyoifungua mahakamani hapo ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa Shauri hilo bado halijaanza kusikilizwa mawakili wa pande zote mbili wameitwa kwa Jaji Cyprian Mkeha kwa ajili ya taarifa kwa ufupi.

Wanachama wamejitokeza kwa wingi katika Mahakama hiyo wakitaka kushuhudia shauri hilo wakiwa kwenye vikundi mbalimbali wakiwa huku wamevaa sare za chama na wale wa upande wa Wabunge hao wamevalia kawaida.

Awali Wakili wa CHADEMA, Peter Kibatala aliwasilisha ombi mbele ya Jaji Mkeha kuwaita wabunge hao ili waje kuwahoji mahakamani hapo kuhusiana na viapo vyao.

Kwa mujibu wa CHADEMA, Mdee na wenzake wamevuliwa uanachama wa chama hicho Novemba 27, 2020 kwa sababu wamekiuka katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila chama hicho kuwapitisha.

Mbali na Mdee, wengine  ni Grace Tendega, Esther Matiko, Ester Bulaya, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Jesca Kishoa na Nusrat Hanje.

Mafuriko yaleta balaa, Wananchi wahitaji msaada
Nape: Wanahabari wanaweza kujisimamia