Meli kubwa ya mafuta iliyokuwa ikiteketea kwa moto katika ufuo wa bahari ya Sri Lanka imezama baharini.
Wadau wa mazingira nchini Sri Lanka wameelezea wasiwasi wao kuwa, huenda kuzama kwa meli hiyo kunaweza kuleta madhara makubwa katika eneo hilo.
Wamesema tayari viumbe vya asili vimeanza kuathiriwa na mafuta waliyokuwa wakivuta kutoka katika meli hiyo, iliyoteketea kwa moto kwa muda wa siku kumi na tatu mfulilizo.