Mgombea urais kupitia chama cha ACT- Wazalendo Bernard Membe, amekanusha taarifa za kuwa Chama hicho kimeungana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika ngazi ya Urais akisema kuwa yeye ndio Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo.
Kupitia ukurasa wa Twitter unaoaminika kuwa ni wa kwake kwani hajawahi kuukana, Membe ameandika, “Mimi ndiyo Mgombea Urais wa JMT kupitia Chama cha ACT-Wazalendo. Mimi ndiye niliyekabidhiwa Ilani ya Chama hicho kuinadi kote nchini kwenye Uchaguzi huu”.
Selfie za kifo: Aanguka nje ya dirisha la gari likiwa kasi akijirekodi video
Kauli ya Membe inakuja baada ya Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad kumuidhinisha Tundu Lissu (CHADEMA), kuwa Mgombea wao wa Urais wa Tanzania.
Mapema mwezi huu mgombea urais wa Tanzania kupitia CHADEMA Tundu Lissu alisema kuwa chama chao kimempitisha Maalim Seif kuwa mgomnea urais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na kuwa hakina mgombea urais Visiwani humo.