Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa wametofautiana kimtazamo na Rais wa Marekani, Donald Trump kuhusu masuala kadhaa muhimu ya kimataifa, ukiwemo mgogoro kati ya Marekani na Korea Kaskazini.

Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na shirika la utangazaji la Ujerumani DW, ambapo amesema ni lazima mzozo wa Korea Kaskazini usuluhishwe kwa njia za kidiplomasia. na Ujerumani inaweza kuwa msuluhishi katika mzozo huo.

Merkel ameikosoa hotuba iliyotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa dhidi ya vitisho alivyovitoa kuwa anaweza kuingamiza Korea Kaskazini kama itaendelea na mpango wake.

”Napinga vitisho vya aina zote. lazima niseme maoni yangu binafsi na ya serikali, ni kwamba suluhisho la kijeshi halifai, tunapendelea juhudi za kidiplomasia. hili lazima litekelezwe kwa dhati. Kwa maoni yangu, vikwazo na kutekeleza vikwazo hivyo ni jibu sahihi. kitu kingine zaidi kuhusu Korea Kaskazini nadhani ni makosa na ni kwa sababu hiyo tunatofautiana kabisa na rais wa Marekani.” amesema Kansela Merkel.

Hata hivyo, Ujerumani ni miongoni mwa nchi chache ambazo bado zina ubalozi katika mji mkuu wa Korea Kaskazini, Pyongyang, na pia ubalozi wa nchi hiyo mjini Berlin, huku pia ikiwa na mahusiano mazuri na China, Japan, Korea Kusini na Marekani.

 

Video: Msigwa aelezea magumu aliyopitia Tundu Lissu, Haponi mtu
Binti mdogo akutwa kifusini akiwa hai