Kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump aliyoitoa wakati akihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa ya kusema ataiangamiza Korea Kaskazini kama itaendelea na mpango wake wa nyuklia imekuwa gumzo na kuzua mijadala mbalimbali kwa wanadiplomasia na watu mbalimbali mashuhuri duniani.

Hotuba ya Rais, Donald Trump wa Marekani katika mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alisema kuwa Marekani ipo tayari kuiangamiza Korea Kaskazini endapo itahitajika kujilinda pamoja na washirika wake,

Aidha, kauli hiyo imeendelea kuibua mijadala miongoni mwa viongozi na wachambuzi mbalimbali wa masuala ya diplomasia na siasa swali likiwa ni je ni kitisho kutokana na sera ambayo Marekani imechukua ama imedhamiria?

Maafisa na wachambuzi kutoka Bara la Asia wamesumbuka usiku kucha wakiwaza kauli hiyo aliyoitoa Trump kuwa ataiangamiza kabisa Korea Kaskazini endapo Marekani itachokozwa.

 

Miili ya watu 13 waliofariki katika ajali ya gari Uganda yaagwa
Mwizi alipongeza Jeshi la Polisi baada ya kumkamata