Miili ya watu waliofariki katika ajali ya gari liliyotokea Jijini Kampala nchini Uganda imeagwa hii leo Jjijini Dar es salaam na kuelekea katika mikoa mbalimbali kuhifadhiwa na ndugu zao.

Aidha watu hao walipata ajali wakitoka kwenye harusi nchini Uganda, mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu 13 papo hapo na wengine 6 kujeruhiwa.

Miili hiyo ya marehemu iliwasili jana usiku na shirika la ndege la Uganda na kupokelewa na Jeshi la wananchi pia kuhifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo ya Jeshi la wananchi iliyopo wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam,

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 21, 2017
Kauli ya Trump kuiangamiza Korea Kaskazini yazua mijadala