Mwizi mmoja nchini Guinea amelipongeza Jeshi la Polisi nchini humo mara baada ya kumkamata kwa kutumia njia za Kamera ambazo wakati akiiba zilikuwa zikimrekodi bila yeye kujua kisha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Boubacar Diallo, mwanafunzi wa Chuo cha ufundi cha Mamou, na mwizi mwenzake wamekiri wenyewe kwamba waliiba kiasi cha franga milioni 50 pesa za Guinea sawa na dola 5,600 kutoka kwenye duka la simu eneo la kaskazini magharibi mwa mji huo.

Aidha, mara baada ya kukamatwa na jeshi la polisi na picha za video kusambaa katika mitandao, Diallo ametoa wito kwa serikali ya Guinea kuliwezesha jeshi hilo kuwa na vifaa vya kisasa zaidi kwaajili ya kupambana na wahalifu kwani wameonyesha uwezo wa juu kumkamata.

“Mkuu wa polisi nchini humu anapaswa kupongezwa, pia ninataka kusema kwamba polisi wanahitaji vifaa vya kisasa zaidi kwasababu polisi yetu ina maafisa wenye mafunzo mazuri, si mchezo, sikutegemea kama wangweza kunikamata,”amesema Diallo

Hata hivyo, ameongeza kuwa hakuwahi hata siku moja kufikiria kwamba ipo siku anaweza kukamatwa haraka na akasema anajuta kwa uhalifu wake pia ameapa kutoiba tena.

Kauli ya Trump kuiangamiza Korea Kaskazini yazua mijadala
Bila Tottenham kufanya hivi Kane anatimka