Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi limeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC kuimarisha ulinzi kwa wakimbizi na wanaoomba hifadhi na si kuwapiga risasi na kuwauwa wakimbizi 39 kutoka nchini Burundi kama wanavyofanya wanajeshi wa Congo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press-AP, limesema kuwa watu wengi waliokufa katika shambulio hilo ni pamoja na watu 94 waliojeruhiwa walikuwa wakimbizi pamoja na wanaotafuta hifadhi kutoka nchini Burundi .

Aidha, kufuatia tukio hilo la mauaji ya wakimbizi, Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na ufyatuaji risasi uliotokea Ijumaa ambapo idara ya wakimbizi imesema watu hao walianza maandamano ya amani kufuatia kukamatwa kwa baadhi ya Warundi.

Hata hivyo, Mkuu wa Idara ya wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, Filippo Grandi amesema kuwa tukio hilo ni baya na halikutakiwa kutokea na ameitaka Serikali ya Congo kuanzisha uchunguzi wa kina.

Shirika hilo linaloshughulikia wakimbizi limesema kuwa hali huko Kamanyola mashariki mwa Congo bado ni tete na zaidi ya Warundi 2,400 wanatafuta hifadhi karibu na kambi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Nyalandu aweka kambi Nairobi kusubiri ruhusu ya kumpeleka Lissu Marekani
Tetemeko la ardhi laua mamia, laporomosha maghorofa