Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire ameomba kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni siku moja mara baada ya kuwekwa mahabusu.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Igogo, ambapo Rais Dkt. Magufuli alimpa nafasi ya kusalimia wananchi, meya huyo ambaye alikamatwa juzi Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati wa kumpokea mkuu wa nchi aliamua kudokeza ya moyoni kwa kuomba faragha.
“Pamoja na kulitolea maelekezo suala la usuluhishi wa mgogoro kati yetu viongozi, mheshimiwa Rais naomba miadi ya kuonana na wewe binafsi ili nikueleze niliyonayo moyoni, ambayo siwezi kuyasema hapa kwenye umati,”amesema Bwire
Aidha, juzi Rais Dkt. Magufuli aliwataka viongozi wa jiji la Mwanza kumaliza tofauti zao kwa njia ya mazungumzo badala ya kufikishana katika vyombo vya dola, kitu ambacho si kizuri.
-
Video: Makonda kukarabati mabasi ya vyombo vya Ulinzi na Usalama Dar
-
JPM: Majizi yote yanakimbilia Chadema
-
Taasisi kujengewa uwezo wa udhibiti wa kemikali na taka sumu
Hata hivyo, hatua hiyo imefikiwa mara baada ya kuwapo kwa mgogoro wa muda mrefu kati ya meya wa jiji la Mwanza, James Bwire na Mkurugenzi wa jiji hilo, Kiomoni Kibamba.