Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto katika suala zima la usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu, ambazo zimekuwa tishio kwa Wananchi hasa Wanawake na Watoto.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi alipokua akifungua warsha ya uzinduzi wa mradi wa kujenga uelewa kwa Taasisi za Serikali katika udhibiti na usimamizi wa kemikali na taka sumu jijini Dar Es Salaam.

Aidha, Muyungi ametoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) kwa msaada wa kifedha katika kuanzishwa kwa mradi huo, hivyo amewataka wajumbe kuitumia vyema elimu watakayoipata katika sehemu zao za kazi ili kuongeza weledi na maarifa.

Hata hivyo, kwa upande wake Mwakilishi kutoka UNEP. Nalimi Sharma amesema kuwa amefurahishi sana kuhudhuria uzinduzi wa warsha ya mradi huo na kuona jitihada mbalimbali zinazochukuliwa katika suala zima la usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu.

 

Video: Lissu 'Karibu Nyalandu', Meya mwenye siri nzito amtaka Magufuli faragha
JPM: Majizi yote yanakimbilia Chadema