Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi ndani ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akisema watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Ameyasema hayo akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

“Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa ndani ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele,”amesema Rais Dkt. Magufuli 

Taasisi kujengewa uwezo wa udhibiti wa kemikali na taka sumu
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 1, 2017