Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, amesema kuwa ana mikakati thabiti ya kuboresha miundombinu yenye changamoto dhidi ya mafuriko na majanga mbalimbali yanayolikumba jiji hilo.

Mwita ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na ugeni kutoka taasisi inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya tabianchi duniani (C40 CITIES) ofisini kwake.

Amesema kuwa wamekubaliana kuleta mtalaamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi ambaye atafanya kazi ya kushughulikia changamoto mbalimbali zinazohusiana na masuala ya mabadiliko jiji.

“Jiji letu linakua kwa kasi kubwa, tunatakiwa kujipanga mapema, maeneo mengi yanakumbwa na mafuriko wakati wa mvua, wananchi wetu wanahangaika, sasa imefika kipindi ambacho tunapaswa kulipatia ufumbuzi jambo hili,” amesema Meya Mwita.

Hata hivyo,  kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa C40 CITIES, Hastings Chikoko, amesema kuwa wamekuja jijini hapa kwa ajili ya kusaidiana katika maeneo matatu ambayo ni usafiri jijini, kukabili mafuriko na ukame ili kuwezesha kilimo cha mijini.

 

CIA waichambua akili ya kiongozi wa Korea Kaskazini
Lowassa awafungukia waliokatwa CCM, ‘jina langu linatajwa’