Wilhelm Heinrich Immanuel Bleek ni mwanaisimu na mwandishi Mjerumani aliyeishi nchini Afrika Kusini.
Anajulikana hasa kwa kuandika kitabu cha sarufi ya Kizulu pamoja na tafiti nyingi za lugha za Kibantu. Neno Bantu, maana yake ni watu
Bleek aliyeishi tangu mwaka mwaka 1827 hadi 1875 ndiye aliye linganisha sarufi za lugha mbalimbali za Kibantu na kuziunganisha, na baadaye Carl Meinhof alimfuata katika utafiti huo.
Lugha za Kibantu ni kundi la lugha ambalo ni tawi la lugha za Niger-Kongo.
Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za Nigeria, Kamerun, Guinea ya Ikweta, Gabon, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Komori, Msumbiji, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Angola, Namibia, Botswana, Lesotho, Swaziland na Afrika ya Kusini.
Uenezi huo unaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa barani Afrika, na idadi ya wanaozitumia ni takriban watu milioni 310.