Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema Mfumo wa Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HRA), hauna lengo la kumuondoa kazini ama kuwaonea watumishi wa umma hivyo hawana sababu ya kuuhofia mfumo huo.

Kikwete amebainisha hayo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa Watumishi wa umma kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Shirika la Masoko Kariakoo na Bodi ya Sukari Tanzania.

Amesema lengo la mfumo huo ni kuiwezesha kupima utendaji wa Watumishi wake kwa njia rahisi na kuongeza ufanisi wenye tija kazini na kuongeza kuwa hauna lengo la kukomoa watu, tunatakuwa na utumishi wa umma unaotimiza majukumu, utawezesha kupamga utumishi wenye tija, huna sababu ya kuhofia.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete

Aidha aliipongeza MOI kwa kutoa huduma bora kwa Watanzania na kuitaka kuendelea na kasi hiyo kwa maslahi ya umma na kwamba mifumo hiyo, inakwenda kuonesha wapi kwenye mapungufu ili paweze kuboreshwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi akimkaribisha Naibu Waziri huyo alimpongeza kwa kuitembelea MOI mara kwa mara na kwamba hatua hiyo inaongeza ari kwa watumishi kufanya kazi kwa umahiri.

Serhou Guirassy agauka lulu Ujerumani, England
Reece James asaka suluhu ya tatizo