Mgombea Urais wa Kenya William Ruto amekataa kushiriki mahojiano ya pamoja ya wagombea wote akisema maandalizi wa tukio hilo wanaengemea upande wa Raila Odinga.
Katika taarifa Julai 14, mmoja wa maafisa wa mawasiliano wa Ruto, Emmanuel Talam alisema waandalizi wa mahojiano hayo wanaegemea upande mmoja na ni wazi kuwa hata kamati ya vyombo vya habari nchini humo imeonyesha wazi kuwa inaunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi wa urais Agosti 9.
Alisema Ruto kuhudhuria kikao hicho ni kumsafishia Raila kama mgombea wa urais.
Hayo yanajiri wakati ambapo ripoti ya MCK ilisema kuwa wanahabari wanapenda kufuatilia habari za Raila ikilinganishwa na Ruto.
“Wanahabari hawajakuwa wakipendelea upande huo kwa sababu ya kutolewa kutoka mikutano ya Ruto kama vile kikao cha wajumbe na wakati wa mkutano Njoro,” MCK walisema katika ripoti.
Katika upande mwingine Naibu Rais William Ruto ametetea hasira yake akisema jinsi nchi inavyoendeshwa haiwezi kuruhusu mtu kuwa na furaha akisema ana hasira kwa sababu nchi inaelekea pabaya.
Mgombea urais huyo wa Muungano wa Kenya Kwanza alikosolewa vikali baada ya kuonekana kwenye video akimkemea Mkenya aliyekuwa amejitokeza kwenye mkutano wake wakati wa kampeni yake.
Akizungumza katika Kaunti ya Kisii mnamo Jumatano, Julai 13, Ruto alisema hasira yake ni kwa sababu nchi inaelekea pabaya, na kuwaacha Wakenya wengi wakiteseka.
Wakenya wamesema Rais wa Muungano wa Kenya Kwanza William Ruto, alikashifu wapinzani wake kwa kukejeli mateso ambayo Kenya inapitia badala ya kujadili masuala muhimu.
“Nataka kuwaambia washindani wetu, tusiongee nani ana hasira na nani hana, kinachoendelea Kenya ni kikubwa, watu wa Kenya hawawezi kumudu chakula, bei ya bidhaa za msingi imepanda. Wakenya wengi hulala njaa hilo si jambo la kufurahisha na ndiyo maana baadhi yetu tuna wasiwasi. Acheni kutuambia kuwa tumekasirika, bila shaka tumekerwa na yanayoendelea nchini,” alisema.
Kitendo hicho cha William Ruto kumtolea maneno ya shutuma kijana alieyehudhuria mkutano kilizua shutuma nyingi, wengine wakisema hasira yake si nzuri kwa mgombea urais.