Katika kutekeleza Sheria ya usimamizi wa maafa, ofisi ya Waziri Mkuu imeanza kuimarisha uratibu wa shughuli za udhibiti wa jambo hilo kwa kuhakikisha uwepo wa mfumo thabiti kwa ngazi zote husika.

Mkurugenzi idara ya menejimenti ya maafa ya ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali Michael Mumanga ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa jukwaa la wadau wa udhibiti wa maafa kwa ajili ya kujadili na kudhibitisha mpango wa Taifa wa kujiandaa na kukabiliana na maafa.

Amesema lengo la jukwaa hilo ni kutoa fursa kwa wadau kutoa maoni yao ikiwemo kuboresha na kuthibitisha mpango ulioandaliwa.

Mkurugenzi idara ya menejimenti ya maafa ya ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali Michael Mumanga akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika jijini Arusha.

Jenerali Mumanga anasema “kutokana na kuongezeka kwa matukio ya majanga ambayo yamekuwa yakisababisha maafa Serikali kwa kushirikiana na wadau wameona umuhimu wa kuwa na mipango mikakati yenye lengo la kujiandaa na kupunguza vihatarishi vya maafa,”

Mipango mikakati hiyo, ni kuhakikisha ni namna gani nchi itawajibika katika kutatua au kupunguza maafa hayo pindi maafa yanapotokea.

Kwa upande wao Wadau wa maendeleo wamesema kukutana kwa wataalam hao na kujadili namna ya kupunguza athari za majanga kutasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Wadau wa maafa katika kongamano lililofanyika jijini Arusha, wakiwa katika makundi kujadili namna ya kukabiliana na maafa pindi yanapotokea.

Mpango huu wa Taifa wa kujiandaa na kukabiliana na maafa, ulianza mwaka 2012 kwa kuzishirikisha taasisi mbalimbali za Kiserikali na binafsi.

Wanafunzi waomba kuishi shuleni na watoto wao
Mgombea Urais akataa kushiriki mahojiano