Mwanamume mmoja, amefariki baada ya kumaliza chupa nzima ya Jagermeister ndani ya dakika mbili pekee, ambapo kabla ya kukumbwa na umauti alikimbizwa Hospitali kwa ajili ya kuokoa masiha yake baada ya kuzimia lakini haikuwezekana.

Mwanamume huyo, anayekisiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30, alipata madhara baada ya kumaliza kinywaji hicho wakati wa shindano la unywaji pombe katika baa ya Brig Motlafela iliyopo eneo la Limpopo, nchini Afrika ya Kusini.

Kupitia video, ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwanamume huyo anaonekana akinywa kinywaji hicho bila kushusha chupa chini huku watu waliokuwa karibu naye wakipiga makofi na kushangilia wakati wa shindano hilo hatari la unywaji pombe.

Kijana anayedaiwa kufariki kwa kunya pombe nyingi kwa mara moja wakati wa shindano la unywaji pombe nchini Afrika ya Kusini.

Mashuhuda wanasema, “alikunywa chupa nzima bila mapumziko hata mara moja ndani ya dakika mbili kabla ya kuzimia kutokana na hali iliyompata ya kupita kiasi, ambapo washindani waliwekewa pesa ikiwa wanainywa chupa ya Jagermeister chini ya dakika mbili.”

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi wa Limpopo nchini Afrika Kusini, imesema uchunguzi juu ya kifo cha kijana huyo unaendelea ili kupata ukweli na kuchukua hatua ambapo shuhuda mmoja anasema alianguka mara moja na alithibitishwa kuwa amefariki baada ya uchunguzi wa Daktari.

Shirika huru la usaidizi wa vileo, Drink Aware linasema unywaji wa kupindukia kunywa pombe nyingi kwa muda mfupi ni jambo ambalo linaweza kusababisha hatari na kuleta madhara au kifo.

Aina yapombe inayodaiwa kushindanishwa wakati wa shindano hilo lililoondoa uhai wa Kijana huyo Afrika ya Kusini.

Nalo Shirika la kutoa misaada la elimu la jijini Cape Town nchini Afrika ya Kusini, linasema mwili wa binadamu unaweza kuchakata takribani kipimo kimoja cha pombe kwa saa moja na chini ya hapo kwa baadhi ya watu.

Msioelewa mtaelewa mbele ya safari: Mwinyi
Vigogo walionunua ardhi Mwanza kuchunguzwa