Mahakama Kuu ya jijini Banjul nchini Gambia, imewahukumu kifo wanachama watano wa zamani wa idara ya upelelezi, kwa mauaji ya mwanaharakati wa kisiasa wakati wa utawala wa dikteta wa zamani Yahya Jammeh.

Jaji wa Mahakama Kuu Kumba Sillah Camara ametoa hukumu hiyo dhidi ya mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Taifa, Yankuba Badjie baada ya kumpata na hatia ya kumuua Ebrima Solo Sandeng, mtu muhimu katika chama cha upinzani cha United Democratic Party, mwaka 2016.

Badjie pia alipatikana na hatia ya kudhuru mwili huku aliyekuwa Mkuu wa operesheni wa shirika hilo, Sheikh Omar Jeng na maafisa wa NIA Babucarr Sallah, Lamin Darboe na Tamba Mansary, walkikutwa na hatia kwa mashtaka hayo hayo na kuhukumiwa kifo.

Kiongozi wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh.

Sandeng, alikamatwa wakati wa maandamano ya Aprili 2016 dhidi ya Jammeh na alifariki akiwa kizuizini siku mbili baadaye ikidaiwa kifo chake kilitokana na kupigwa na kuteswa.

Madai ya kifo cha Sandeng, yalichochea vuguvugu la kisiasa ambalo hatimaye lilimuondoa madarakani Jammeh, ambaye alikuwa ametawala taifa hilo dogo la Afrika Magharibi kwa miaka 22.

Afisa mwingine wa NIA, Haruna Susso na Nesi mmoja, Lamin Sanyang wao hawakupatikana na hatia ya mauaji au kudhuru mwili katika mashikata hayo.

Mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Taifa nchini Gambia, Yankuba Badjie aliyehukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanasiasa, Ebrima Solo Sandeng.

Naibu mkurugenzi wa zamani wa shirika la kijasusi, Louie Richard Leese Gomez, pia alikuwa ameshtakiwa lakini amefariki dunia huku afisa mwingine, Yusupha Jammeh, alikuwa ameshtakiwa lakini baadaye akaachiliwa huru.

Hali ilivyokuwa katika viunga vya Mahakama kuu, nchini Gambia

Mgombea Urais akataa kushiriki mahojiano
Msioelewa mtaelewa mbele ya safari: Mwinyi