Operesheni ya ukamataji wa Madawa ya kulevya Nchini kwa mwaka 2022 zilifanikisha kukamata tani 15 za mirungi, kilo 254.7 za heroin na kilo 1.7 ya cocaine.
Akizungumza hayo hii leo Bungeni Jijini Dodoma, Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama wakati akitoa taarifa kuhusu hali ya dawa za kulevya ya Mwaka 2022.
Amesema, “bangi imeendelea kuwa ni dawa inayotumika zaidi Nchini, mwaka 2022 Serikali ilifanikiwa kuteketeza hekari 179 za mashamba ya bangi na tani 20.58 za dawa hizo ambazo zilikamatwa katika Mwaka huo”, amesema.
Mhagama ameongeza kuwa, “hivi karibuni kumeibuka tabia ya changanya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi kwenye vyakula kama vile biskuti, keki, juisi, asali na majani ya chai”.Amesema Muhagama
Hata hivyo, amesema taarifa ya dawa za kulevya Duniani mwaka 2022 inaonyesha kuwa 40% ya Nchi zenye matumizi makubwa ya madawa ya bangi zilikumbwa na idadi kubwa ya magonjwa ya afya ya akili uhalifu na uvunjifu wa amani yaliyosababishwa na dawa hizo.
Aidha, amesema Serikali imefanikiwa kuandaa mwongozo wa utoaji elimu juu ya tatizo hilo la dawa za kulevya Nchini lengo ni kuhakikisha jamii inapata elimu sahihi juu ya tatizo hili.