Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Sadick Malila ameshtushwa na taarifa zilizotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa kuhusu zuio la ufanyaji ibada maalumu iliyoandaliwa kumwombea Lissu, kutokana na tetesi zinazoelezea kuwa hali yake bado tete nchini Kenya.
Kamanda wa Polisi, George Kyando ametoa tamko la zuio hilo kwa madai ya kwamba viongozi wa chama hicho(CHADEMA) hawakuomba kibali kwa kamanda wa polisi wa Wilaya ambaye angeruhusu kufanyika kwa ibada hiyo.
Hivyo baada ya kauli ya uamuzi huo kutoka kwa kamanda wa polisi, ilimlazimu Mwenyekiti Chadema kusitisha zoezi hilo la kufanya maombi na kuwasihii wananchi kila mtu atumie muda wake binafsi kumwombea Lissu.
Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria, alishambuliwa na risasi mjini Dodoma na watu wasiojulikana wakati akiwasili nyumbani kwake Area D akitokea bungeni siku ya Alhamisi y wiki iliyopita.
Jana Mkuu wa Idara ya Uenezi Chadema, Hemed Ali amesema ‘ Hali yake bado ni mbaya ila maendeleo ya kuwa vizuri yanaelekea kuw achanya ila ameumizwa sana , kwani risasi alizopigwa zilisababisha kumvunjavunja mguu, mkono wa kushoto na nyonga’’. Amemaliza hivyo.