Timu ya taifa ya Syria itakua mwenyeji wa mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya mtoano kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia 2018 dhidi ya Australia mwezi Oktoba.

Timu ya taifa ya Syria ambayo haijawahi kufuzu fainali za kombe la dunia, itacheza mchezo huo katika mji wa Melecca nchini Malaysia, kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea nchini kwao.

Tayari shirikisho la soka soka nchini Malaysia limethibitisha mchezo huo kuchezwa katika ardhi ya nchi hiyo kama ilivyokua katika michezo ya awali iliyoihusu Syria ya harakati za kufuzu fainali za kombe la dunia.

Hata hivyo shirikisho la soka nchini Australia nalo limekubali mchezo huo wa mkondo wa kwanza kucheza mjini Melecca.

Shirikisho la soka duniani FIFA lilipiga marufuku michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia kuchezwa katika mji wa Damascus kutokana na vita inayoendelea katika mji huo.

Mshindi wa michezo ya mikondo yote miwili kati ya Australia na Syria atacheza dhidi ya mshindi wa tano kutoka ukanda wa Amerika ya kati na kaskazini ili kumpata atakaefuzu moja kwa moja kwenye fainali za kombe la dunia za 2018 zitakazochezwa nchini Urusi.

Misa ya kumwombea Lissu yazuiliwa
Wabunge Uganda wataka kuondoa ukomo wa urais