Shehena muhimu ya misaada ya kibinadamu imewasili katika mji wa Port Sudan, huku mapigano yakizidi kushika kasi kati ya jeshi la Sudan na kundi pinzani la wanamgambo wa RSF.

Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu – IFRC, limesema misaada hiyo inajumuisha blanketi, vifaa vya jikoni na vyandarua, kwa familia 500 huku shehena nyingine ikiwemo vifaa vya matibabu ikitarajia kuwasili hivi karibuni.

Shirika la Afya Duniani – WHO, linaema tangu kuzuka kwa mapigano hayo zaidi ya mwezi mmoja uliopita, takriban watu 600 wameuawa huku zaidi ya watu 700,000 ndani ya Sudan wakikosa makazi na wengine 200,000 wakikimbilia nchi jirani.

Jeshi la Sudan, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, linapambana na Vikosi vya wanamgambo, vinavyoongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo wakigombania kushika madaraka.

Thamani uwekezaji mifuko hifadhi ni Trilioni 1.4 - Katambi
Matukio ukatili wa kijinsia yashika kasi Kilimanjaro