Siku kadhaa baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kutangaza kutengua adhabu ya kulifungia shindano la Miss Tanzania, uongozi wa shindano hilo umetangaza kamati mpya.

Kamati hiyo yenye wajumbe 12 iko chini ya uenyekiti wa Juma Pinto na imeahidi kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha mapungufu yaliyojitokeza awali hayajitokezi tena.

Akiongea na waandishi wa habari, msemaji wa kamati hiyo, Jokate Mwegelo ameeleza kuwa kamati hiyo imeyapokea majukumu yake na kuahidi kusimamia sheria, kanuni na taratibu za mashindano hayo huku akiiomba jamii iendelee kuwaunga mkono kwa lengo la kuendeleza tasnia ya urimbwende nchini.

Jokate Mwegelo

Jokate Mwegelo

“Leo hatutakuwa na mengi ya kueleza kwa kuwa ndio kwanza tumekabidhiwa jukumu hili, kamati yetu itakutana kupanga mipango na mikakati endelevu ya kuendeleza sanaa hii ya urembo ndani hadi nje ya mipaka ya Tanzania,” alisema Jokate.

Haya ni majina ya wajumbe wa kamati hiyo mpya:

1.Juma Pinto – Mwenyekiti

2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti

3.Doris Mollel – Katibu Mkuu

4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati

5.Hoyce Temu – Mjumbe

6.Mohamed Bawazir – Mjumbe

7.Gladyz Shao – Mjumbe

8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe

9.Shah Ramadhani – Mjumbe

10.Hamm Hashim – Mjumbe

11Khalfani Saleh – Mjumbe

12.Ojambi Masaburi – Mjumbe

Bondia Wa Kike Anaetamba Kumpiga Mayweather Amchokoza Na Pesa
NEC Yaingilia Kati Ukawa Kutumia Uwanja Wa Jangwani