Mbunge wa Ulyankulu, Rehema Migila amesema mtu anayetengeneza mkaa, hutumia miti tani 10-12 ambapo anapata mkaa wa kawaida wenye wastani wa tani 1 pekee.
Migila ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Nishati Juni Mosi, 2023.
Amesema, “kuna tafiti mimi nimefanya kidogo. Inaonesha kwamba mtu anayekata mkaa, hutumia miti tani 10-12 ambapo anapata mkaa wa kawaida wenye wastani wa tani 1, tunaona namna gani wanavyoharibu mazingira na miti inakwisha.”
Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo ameiomba Wizara ya Nishati kuanzisha mashamba darasa ya kupanda miti inayokuwa haraka.