Kwa mara ya kwanza Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa, Karim Benzema amefunguka juu ya ishu ya yeye kuhusishwa kutaka kuondoka ndani ya Real Madrid kwa kusema kwa sasa bado yupo ndani ya kikosi hicho.

Benzema alitoa kauli hiyo baada ya wiki hii kuhusishwa kuomba kuondoka ndani ya miamba hiyo ya Hispania ambayo amedumu nayo kwa misimu 14 akibeba mataji mbalimbali yakiwemo ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ na Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’.

Nyota huyo anahusishwa kutaka kujiunga na Klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia ambayo imemuwekea dau nene kwa ajili ya kujiunga nao.

Benzema amesema: “Mnazungumza na mashabiki wa Madrid kuhusu kubakia kwangu hapa? Kwa nini? Kwa nini mzungumzie kuhusu wakati ujao wakati bado nipo hapa Madrid,

“Wanasema dili hilo limekamilika? Lakini nani anayesema, ni mtandao… ukweli siyo mtandao.”

Wachezaji Young Africans wakabidhiwa majukumu
Uharibifu: Miti tani 12 hutoa mkaa tani moja - Mbunge Migila