Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi, amesema kuwa ni muhimu wachezaji wote kuongeza umakini wakiwa ndani ya 18 pamoja na wakipoteza mpira kukaba kwa wakati ili kupata ushindi kwenye mechi yao dhidi ya USM Alger leo Jumamosi (Juni 03) nchini Algeria.

Hayo ni majukumu mengine kwa nyota wake wote ikiwa ni pamoja na mshambuliaji namba moja, Fiston Mayele mwenye mabao saba na pasi mbili kimataifa, beki Yannick Bangala kiraka Mudathir Yahya pamoja na Farid Mussa.

Timu hiyo leo Jumamosi (Juni 03) inatarajiwa kumenyana na USM Alger ikiwa ni mchezo wa fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ule wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Young Africans 1-2 USM Alger.

Kocha Nabi amesema kuwa wanatambua ugumu uliopo kuwakabili wapinzani nyumbani lakini ni lazima kila mchezaji kuwa makini kwenye mchezo huo.

“Wapinzani wetu tunawaheshimu na hilo ni muhimu kwa kila mchezaji kwenye timu kuwa makini pale anapokuwa ndani ya 18 na mpira na anapopoteza mpira hilo litafanya tuongeze hali ya kujiamini.

“Kupoteza kwa mchezo wetu uliopita hakuna ambaye alipenda lakini imetokea na tuna kazi nyingine kuwakabili, hilo lipo wazi sitaki kuahidi kwamba tutapata ushindi kirahisi ila tunahitaji kupata ushindi,” amesema Nabi

Young Africans imefunga mabao 16 huku ukuta ukiruhusu kufungwa mabao saba ugenini.

Wahusika uhalifu wa Binadamu waundiwa mkakati
Karim Benzema avunjwa ukimya Real Madrid