Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita – ICC, Karim Khan wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kutowachukuliwa sheria watu wanaohusishwa na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Hatua hiyo, imefikiwa kufuatia ziara ya siku nne ya Khan  nchini Kongo ambapo  amesema pamoja na kuwepo ushirikiano mzuri kati ya ICC na DRC lakini bado kuna visa vingi vya uhalifu na unyanyasaji dhidi ya wanaume na wanawake kubakwa.

Amesema, “kwa bahati mbaya wasichana wengi, wavulana na wanawake wanaendelea kunyanyaswa na kubakwa. Nimewaona waathirika wa visa hivyo. Nimewaona watoto waliobakwa na kujifungua watoto ambao nao pia walibakwa. Na mzunguko huo utaendelea ikiwa hatutojenga ushirikiano mpya.”

Mahakama ya ICC imekuwa ikiifuatilia DRC tangu mwaka 2002 na ilianzisha uchunguzi wake wa kwanza kaskazini Mashariki mwa jimbo la Ituri mwaka 2004. ICC na Kongo jana walisaini mkataba wa maelewano wa kushirikiana.

Cristiano Ronaldo atumika Saudi Arabia
Wachezaji Young Africans wakabidhiwa majukumu