Mshambuliaji wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo amewaita mastaa mbalimbali kwenda kucheza Ligi ya Saudi Arabia kwa kuwa ligi ya nchi hiyo ni nzuri.

Ronaldo ametoa kauli hiyo baada ya mastaa mbalimbali wa Ulaya wamekuwa wakihusishwa kutakiwa na klabu za nchi hiyo akiwemo mpinzani wake Lionel Messi.

Ronaldo amesema: “Nina furaha hapa Al Nassr ninataka kundelea kukipiga hapa sababu ninajiamini kuwa hapa. Maisha ya Saudi yanaendelea vizuri na pia ligi ni nzuri.

“Ninawakaribisha wachezaji wakubwa, pia wale wenye majina makubwa au vijana wadogo. Kama hilo litatokea basi ligi itaimarika.”

Robertinho afunguka saa 120 Simba SC
Wahusika uhalifu wa Binadamu waundiwa mkakati