Baada ya kikosi chake kurejea kambini juzi Alhamisi (Juni Mosi), Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Olivieira ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa wameandaa programu ya mazoezi ya siku tano sawa na saa 120 kumaliza hesabu zao za msimu huu na kuanza rasmi maandalizi ya msimu ujao.

Simba SC wamesaliwa na michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Juni 6, mwaka huu kabla ya kumalizana na Coastal Union Juni 9, mwaka huu.

Kwenye msimamo, Simba SC wanakamata nafasi ya pili na alama zao 67 walizokusanya kwenye michezo 28 waliyocheza, wakishinda mechi 20, sare saba na kupoteza mchezo mmoja.

Simba SC inaendelea na mazoezi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Simba MO Arena chini ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 pamoja na wasaidizi wake.

Robertinho amesema: “Jambo zuri kwetu ni kuwa kikosi kimerejea kambini kwa ajili ya kumalizia maandalizi yetu ya michezo miwili iliyosalia na tumeandaa programu ya siku tano kumaliza kabisa hesabu za msimu huu.

“Baada ya michezo dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union ambayo itakuwa mwisho rasmi wa msimu kwetu tunatarajia kutoa mapumziko ya muda kwa wachezaji wote kabla ya kurejea kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Pre Season’ ya msimu ujao.”

Zoezi uhamishiaji Wananchi Msomera halijasimama - Serikali
Cristiano Ronaldo atumika Saudi Arabia