Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya klabu ya Simba, Mulami Ng’ambi amefafanua ujumbe wa mkurugenzi wake wa bodi, Mohammed Dewji baada ya kutweet na kueleza hisia zake juu ya uwekezaji wa mkataba mpya wa klabu ya Manchester United na kuhusisha Simba na mkataba wa SportPesa.
MO aliandika, “Man Utd italipwa kiasi cha pauni milini 305 ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 700 za kitanzania kwa miaka mitano kutoka kwa (Team Viewer). Simba ya Tanzania haipati hata asilimia moja ya hiyo pesa kutoka kwa wadhamini Sportpesa (Asilimia moja ya hiyo pesa ni kiasi cha Bilioni 7 za kitanzania).”
Mulami amesema,”Watu hawakumuelewa Mo Dewji. Alichokimaanisha Mohamed Dewji alikuwa anaamnisha kwamba, hela ambayo ipo au inawekezwa kwenye mpira kama udhamini bado ni kidogo sana kulinganisha na nchi nyingine ambazo zinapata udhamini.
“Nafkiri alisema Simba haipati asilimia moja ya udhamini ambayo Manchester United wanaipata katika mkataba mpya ambao wameisaini hivi karibuni. Manayake ni kwamba ilikuwa ni kuhamasisha makampuni juu ya umuhimu wa kuongeza fedha zao kwenye mpira.”
Hakuwa akimaanisha ni Sportpesa pekeyake, ikumbukwe kulikuwa na makampuni mengi ambayo yalijiondoa katika mpira wetu, NMB, TBL na zaidi. Ukweli ni kwamba fedha inayowekezwa kwa sasa ni ndogo sana ikilinganishwa na thamani ya Simba iliyonayo hivi sasa.amesema Mulamu Ng’ambi, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba.