Muda mfupi baada ya taarifa kuzagaa kwamba boss wa Spurs Mauricio Pochettino huenda akachukua kibarua cha ukocha kwenye klabu ya Manchester United, tarari kuna taarifa zinazosema Jose Mourinho ameshamalizana na klabu hiyo ya Old Trafford.

Gazeti la The Sun limeandika Man United wapo kwenye mazungumzo na wawakilishi wa manager wa Spurs lakini kiuhalisia inasemekana kocha huyo hana wakala.

Magazeti matatu ya Jumatano (leo) yametoka na vichwa vya habari vinavyofanana kila gazeti likidai Jose Mourinho ameshawaambia rafiki zake wa karibu kwamba yeye ni kocha mpya wa Manchester United.

Tangu kocha huyo atimuliwe na klabu yake ya zamani Chelsea, ripoti za Mourinho kuchukua mikoba ya Louis van Gaal mwishoni mwa msimu huu zimezagaa Ureno, Italia, Hispania na sasa England.

Jumapili iliyopita Louis van Gaal alikuja juubaada ya kuulizwa kuhusu hatma yake kunako Old Trafford baada ya Manchester United kuambulia sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Chelsea.

Hivi ni vichwa vya habari vya baadhi ya magazeti yaliyotoka leo huku habari kubwa ambayo imepewa uzito na magazeti yote ni kuhusu Mourinho kutua Man United.

Magazeti 2Magazeti 1Magazeti

Mabingwa Wa Soka Tanzania Bara Waahirisha Safari Ya Mauritius
Bondia Ibrahimu Maokola Ajifua Kumkabili Joseph Sinkala March 12