Kikosi cha timu ya Yanga kilichokuwa kiondoke nchini leo sasa kinatarajiwa kuondoka kwa ndege ya kukodi jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa majira ya asubuhi.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa timu yao itaondoka Ijumaa kwa ndege ya kukodi kuelekea Mauritius kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Cercle de Joachim.

Msafara wa Yanga utajumuishwa kikosi cha wachezaji 21 kati ya 24 waliosajiliwa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Wachezaji walioachwa ni Matheo Anthony, Geoffrey Mwashiuya na Benedicto Tinoco.

Pambano hilo litapigwa siku ya Jumamosi majira ya saa nane na nusu kwa saa za Tanzania sawa na saa tisa na nusu kwa saa za Mauritius.

George ‘Best’ Nsimbe: Ninaifahamu Vizuri Enyimba Ya Nigeria
Mkanganyiko Wa Habari Za Mrithi Wa Louis Van Gaal Old Traffold