Kampuni inayo milikiwa na bilionea Elon Musk, ipo kwenye hatua za mwisho mwisho za kukamilisha mradi wake wa kutengeneza mke roboti, ‘robot wife’ atakayeuzwa sehemu mbalimbali Duniani ili kuwasaidia wanaume usumbufu wa kuoa na kujikuza kiuchumi.
Mradi huo, unatarajiwa kukamilika rasmi Septemba 2023 ambapo wanawake hao watakuwa wanapatikana madukani na wanatarajia kufikishwa Barani Afrika ifikapo Novemba 2023.
Kampuni hiyo inasema mtu atakae mnunua robot awe mke wake atakuwa ameokoa matumizi ya pesa kwa kiasi kikubwa, ukilinganisha na mwanamke halisi.
Mke robot anatumia betri ya kuchajiwa kwa siku tatu mfululizo na kufanya kazi kwa mwezi mmoja ambapo kwa siku hizo (tatu), mwanaume hataweza kushiriki tendo na mke wake (roboti).
Hata hivyo, ili kulala na mke roboti mmiliki atahitaji kuwa na neno maalumu la siri ‘password’, litakalomfanya amtambue kuwa ndiye mumewe na anatarajia kuuzwa kwa zaidi ya Shilingi 7.4 milioni.