Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umefunguliwa mjini Maputo nchini Msumbiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anahudhuria Mkutano huo kwa mara ya kwanza huko Msumbiji tangu alipopata wadhidfa huo Machi Mwaka huu.
Akifungua Mkutano huo, Mwenyekiti wa SADC ambaye ni Rais wa Msumbiji, Philipe Nyusi amemkaribisha SADC Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Mwanamke pekee Rais kwa sasa katika nchi za SADC.
Katika hotuba yake, Rais Nyusi amezitaka nchi za SADC kushirikiana katika kuendeleza mapambamo dhidi ya ugonjwa wa corona, ugonjwa ambao unaendelea kuziathiri hata nchi za Jumuiya hiyo.
Aidha, amewashauri Wakuu hao wa Nchi na Serikali wa SADC kuhakikisha nchi zao zinatoa elimu ya kutosha kwa Wananchi, ya namna ya kijikinga na kukabiliana na ugonjwa huo wa corona.
Rais Nyusi amesisitiza mapambano dhidi ya vitendo vya kigaidi ambavyo navyo vimekuwa vikishamiri katika baadhi ya nchi za SADC.