Jumla ya mashauri 1,208 yamesikilizwa na kumalizwa na Mahakama inayotembea ‘mobile court’ huku watu 13,668 wakiwa wamenufaika na huduma zinazotolewa na Mahakama hiyo katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.

Dar24 Media imefanya mazungumzo na Wakili wa kujitegemea kutoka Avis Legal, Henry Mwinuka kujua maoni yake ni nini kuhusiana na Mahakama inayotembea (Mobile Court), ambapo amesema kwamba kuwa na Mahakama hiyo ni mapinduzi makubwa katika muhimili wa utoaji haki nchini.

Amesema suala la utoaji haki wakati mwingine limekuwa likikabiliwa na changamoto za kimiuondombinu, uchache wa wahudumu na watoa haki wenyewe.

Muonekano wa ndani wa Mahakama inayotembea ‘Mobile Court’

“Kitendo cha Mahakama ya Tanzania kuja na wazo la Mahakama inayotembea itasaidia ni kitu muhimu sana cha kukipigia chapuo,” amesema Wakili Mwinuka.

Aidha, Wakili Mwinuka ameongeza kuwa Mahakama hiyo ina uwezo wa kuwafikia hata walio vijiji vya ndani ambapo Mahakama hazipo lakini mashauri yanakuwepo, hivyo kupitia Mahakama hiyo wananchi wanapata haki zao za msingi.

Mwinuka ameshauri Mahakama kuongeza zaidi Mahakama hizo zinazotembea ili ziweze kutoa hduma ya haki za kibinadamu kwa upana zaidi kwa sababu uhitaji bado ni mkubwa kwa wananchi.

Serikali kujenga kiwanda cha kuzalisha dawa nchini
Recho Kizunguzungu: Niliachwa kisa skendo ya madawa