Tukio la mtoto wa mwaka mmoja na nusu kudaiwa kunyongwa hadi kufa na msichana wa kazi inadaiwa kuwa sio tukio lake la kwanza ambapo tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina .

Kwa mujibu wa gazeti la nipashe, majirani wa eneo la tukio walizungumzia mazingira ya mauaji hayo huku Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkeriyani, Kata ya Olasiti jijini Arusha, Aminiel Mollel, akitoa tahadhari kwa waajiri kufahamu mazingira wanapotokea wasaidizi hao.

Mollel amesema alipata taarifa ya tukio hilo na kwenda kumchukua mtoto huyo hadi Hospitali ya Mount Meru, ambako baada ya uchunguzi waligundua ameshafariki dunia.

“Katika kumhoji msichana wa kazi alisema huyo ni mtoto wa tatu kumnyonga na wakati anamnyonga hakuwa na akili yake, lakini akishamaliza ndiyo inarudi, tunafikiri ni nguvu za giza zinamwendesha kufanya matukio haya,” amesema Mollel.

“Watu walipofika nyumbani walimkuta anaosha vyombo kama hakuna kilichotokea,” amesema Mollel

Mkutano wa Dharura wa SADC waanza, Rais Samia akaribishwa
Serikali kujenga kiwanda cha kuzalisha dawa nchini