Mkutano wa Jukwaa la Dunia la Uchumi umeanza leo mjini Davos, nchini Uswisi, huku vita vya Ukraine na mdororo wa uchumi duniani zikiwa mada kuu za mazungumzo, ambao pi umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Baada ya hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na mwanzilishi wa jukwaa hilo, Klaus Schwab macho na masikio vilielekezwa kwenye hotuba ya Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen.
Mkutano huo, unakuja wakati Bara la Ulaya likikabiliwa na changamoto zikiwemo athari za uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, na machungu yatokanayo mfumuko wa bei na ukuaji hafifu wa uchumi.
Mke wa Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine, Olena Zelenska ni miongoni mwa watu wengine watakaolihutubia jukwaa hilo ambapo katika ripoti yake ya mwaka juu ya hali ya uchumi wa dunia, amesema kupanda kwa gharama ya maisha na mizozo ya nishati na chakula ndivyo vizingiti vikuu kwa wakati huu.