Hatimaye Shule za awali, Msingi na Sekondari zimeruhusiwa kufunguliwa rasmi na Wizara ya afya nchini Malawi baada ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu ambayo awali yalisababisha kufungwa kwa shule hizo.

Kupitia taarifa yake, Wizara hiyo imeeleza maambukizi ya ugonjwa huo yamepungua kwa kiwango kikubwa na kuruhusu kufunguliwa kwa shule na huduma za jamii kwa baadhi ya maeneo ambazo zilifungwa ili kuepusha usambaaji wa ugonjwa huo.

Wanafunzi wakiwa Darasani. Picha ya Salesiana.

Aidha, taarifa hiyo imezidi kufafanua kuwa baadhi ya shule katika maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa huo wa kipindupindu zitaendelea kufungwa, ili kufuatilia mwenendo wa maambukizi na afya kiujumla na kisha itatoa taarifa zaidi hapo baadaye.

Mapema hivi karibuni, Shirika la afya Duniani (WHO), lilionya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu unaoendelea kuripotiwa kwenye mataifa huku nchi za Malawi, Syria na Lebanon, zikitajwa kuathirika zaidi.

Washauriwa kuwashirikisha Wananchi utambuzi madai ya haki
Mbeya kupata ahueni mradi wa maji mto Kiwira