Mkuu wa Twitter, Jack Dorsey ameweka ujumbe wenye picha ya bendera ya Nigeria mtandaoni katika hatua ambayo vyombo vya habari nchini humo vinaashiria ni kuunga mkono maandamano ya Jumamosi dhidi ya uongozi mbaya na kulalamikia kufungiwa kwa Twitter.
Ujumbe wa Dorsey umewavutia Wanigeria wengi wanaotumia mtandao wa VPN kufikia programu hiyo tumishi.
Twitter inajadiliana na serikali ya Nigeria baada ya kupigwa marufuku nchini humo tarehe 5 mwezi Juni.
IMarufuku hiyo ilifuatia baada ya hatua ya mtandao huo kufuta ujumbe wa Rais Mohammadu Buhari ingawa ofisi yake imesema hatua hiyo haihusiani kivyote na suala hilo.
Raia wa Nigeria siku ya Jumamosi waliandamana kulalamikia uongozi mbaya, ukosefu wa demokrasia na kupigwa marufuku kwa Twitter.
Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanji na kuwakamata baadhi yao,kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
Maandamano ya Jumamosi, ni ya kwanza tangu maandamano ya ‘EndSARS’ ya kupinga ukatili wa polisi yaliyofanywa kwa wiki kadhaa.