Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa amewapongeza wachezaji wake kwa kazi kubwa waliyoifanya jana Jumatano (Mei 04) kwa kukabili Young Africans, Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Ruvu Shooting ilikua mwenyeji wa mchezo huo wa Ligi Kuu ambao umekua mchezo pekee kwa msimu huu 2021/22 kuchezwa mkoani Kigoma, baada ule ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kati ya Simba SC dhidi ya Young Africans kuchezwa uwanjani hapo mwishoni mwa msimu uliopita 2020/21.

Kocha Mkwasa amesema wachezaji wake walifuata maelekezo ya kiufundi na kuyatumia wakati wote wa mchezo huo, na ndio maana walifanikiwa kuibana Young Africans na mwisho wa dakika 90 wakaambulia alama moja.

Amesema wachezaji wake walikua wasikivu sana na walidhamiria kuwa timu ya kwanza kuifunga Young Africans kupitia mchezo huo, lakini bahati haikuwa kwao, japo bao walilofunga lilikataliwa kwa madai ya mfungaji Sadat Mohamed alikua ameotea.

“Wachezaji wangu walicheza kwa kujituma sana, walifuata maelekezo yangu ya kiufundi, ninawashukuru sana kwa hilo kwa sababu kazi waliyoifanya ilikua kubwa sana.”

“Wameonyesha kupambana wakati wote na kila mmoja ameona hali ilivyokua ndani ya Uwanja, inawezekana kwa timu kama Ruvu Shooting kupambana na yoyote katika Ligi yetu, na hivyo ndivyo nimekua niwasisitiza kila siku ili kufanikiwa kufikia malengo yetu.” amesema Mkwasa.

Matokeo ya Mchezo wa jana dhidi ya Young Africans, yameifanya Ruvu Shooting kufukisha alama 22 zinazoiweka katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Kocha Pablo awajibu wadau wa Soka La Bongo
Kocha Pablo: Sina tatizo na Clatous Chama