Washika bunduki wa Ashburton Grove, Arsenal wamepata majanga kufuatia kuumia kwa mchezaji William Carvalho waliokuwa wanamfuatilia katika msimu huu wa usajili.

Taarifa kutoka nchini Ureno zinaeleza kwamba Carvalho anayeitumikia klabu ya Sporting Lisbon, amepata majeraha ya mguu na atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi isiyopungua mitatu.

Uchuguzi wa kitabibu uliofanywa na jopo la madaktari klabuni hapo umoenyesha kwamba Carvalho ambaye alikua sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno chini ya umri wa miaka 21 wakati wa fainali za mataifa ya barani ulaya kwa vijana iliyofanyika Jamuhuri ya Czech mwezi uliopita, amevunjika mfupa wa mguu.

Hata hivyo bado haijafahamika kama Arsenal wataendelea na mipango ya kutaka kumsajili kiungo huyo ama la, kutokana na taarifa za kuumiwa kwa Carvalho, kuthibitishwa usiku wa kuamkia hii leo.

Man Utd nao walikua katika mawindo ya kumsajili kiungo huyo, lakini walijiondoa baada ya kufanikiwa kuwanasa viungo wawili, mwanzoni mwa juma hili Morgan Schneiderlin pamoja na Bastian Schweinsteiger.

Maradona Amshauri Messi
Man Utd Kumruhusu Chicharito Wakiridhishwa