Mashetani wekundu Man Utd, wanatarajia kuijadili ofa ya paund million 8 iliyowasilishwa huko Old Trafford ikitokea Upton Park yalipo makao makuu ya klabu ya West Ham Utd, ambayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Mexico, Javier Hernandez.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amekuwa katika orodha ya wachezaji wanaohitajika magharibi mwa jijini London tangu msimu uliopita, lakini Man Utd walifanya maamuzi ya kumpeleka kwa mkopo Real Madrid.

Man Utd wamethibitisha kuwa katika harakati za makubaliano ya kuuzwa kwa Chicharito kupitia vikao vyao vya ndani na kama itaonekana ofa iliyotua mezani kwao inafaa, wataafiki mshambuliaji huyo kuondoka.

Hata hivyo West Ham Utd wanakabiliwa na upinzani kutoka kwenye klabu kadhaa za barani Ulaya ambazo zimeonyesha nia ya kumuwania Chicharito.

AS Roma, Galatasaray, Besiktas pamoja na Wolfsburg ni miongoni mwa klabu zinazotajwa kuwa katika mipango ya kumsajili Chicharito.

Chicharito amekua na maisha magumu katika kikosi cha Man Utd tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson, kutokana na mifumo inayotumiwa na mameneja waliomfuatia babu huyo.

Mlengwa Katika Usajili Wa Arsenal Apata Majanga
Real Madrid, Espanyol Ngoma Ngumu