Mamlaka za afya nchini Nigeria, zimethibitisha mlipuko mbaya wa matatizo ya kupumua (Dipththeria), katika jimbo la Kano ambalo limeathiriwa zaidi hasa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ambapo hadi sasa kuna vifo 25.
Kwa mujibu wa afisa wa Tume ya Afya ya jimbo hilo, Dkt. Aminu Tsanyawa amesema wamerekodi zaidi ya visa 70 vinavyoshukiwa, pamoja na vifo 25 vinavyohusiana na maambukizi ya bakteria.
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Nigeria, tayari kimeanzisha harakati za dharura ili kukabiliana na mlipuko huo na kinafuatilia hali hiyo katika majimbo manne kati ya 36 ya Taifa hilo.
Ugonjwa huo, husababisha matatizo ya kupumua, kushindwa kwa moyo na kupooza huku watu walio hatarini zaidi ni maeneo ambayo hayana chanjo na yaliyoathiriwa na uchafu.