Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Klabu ya Simba SC Mohamed Dewji ‘Mo’ ameendelea kufanya uteuzi wa Safu ya uongozi wa klabu hiyo, baada ya kufanya hivyo tangu mwanzoni mwa juma hili.

Mo Dewji ambaye amewekaza Simba SC asilimia ya Hisa 49, ametangaza hadharani kumteuwa Crescentius Magori kuwa Mshauri wake katika mambo mbalimbali Michezo ndani ya Klabu hiyo.

Mo ametangaza uteuzi huo kupitia andiko maalum alilolichapisha katika Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii akiandika: “Kufuatia kazi nzuri aliyoifanya Ndugu Crescentius Magori katika kunishauri kuhusu maendeleo ya Klabu yetu ya Simba, nimeteua tena kwa kipindi kingine kuwa Mshauri wangu kuhusu michezo kwa ujumla na maendeleo ya Klabu yetu ya Simba. Hongera Ndugu Magori!”

Jana Jumanne (Februari 28) ‘Mo’ alitangaza kuwateuwa Wajumbe wanne wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC ambao wataungana na Wajumbe wengine waliochaguliwa na Wanachama chini ya Mwenyekiti Salim Abdallah ‘Try Againe’ ambaye anaendelea na majukumu yake klabuni hapo.

Wajumbe walioteuliwa ni Dk. Raphael Chegeni, Mhe Rashid Shangazi, Bwana Hamza Johari na Bwana Zulfikar Chandoo.

Uchaguzi Nigeria: Tinubu Rais mteule, wapinzani wamkataa
Hatimaye Godbless Lema awasili nchini