Alvaro Morata alifunga mabao matatu katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa hapo jana wakati Chelsea ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City.
Morata alifunga bao la kwanza dakika ya 2 baada ya mchezo kuanza akipokea pasi nzuri kutoka kwa Cesar Azpilicueta kabla ya Pedro kufunga bao la pili dakika ya 30 kisha Morata akafunga dakika ya 70 na 82.
Hii ni hat-trick ya kwanza kwa Morata tangu ajiunge na Chelsea kwa ada ya pauni milioni 60 akitokea Real Madrid, mshambuliaji huyo anaonekana kuanza kuonyesha uwezo mkubwa ikiwa ni siku chache baada ya Chelsea kukubali kumuuza Diego Costa.
-
Video: Atletico Madrid yaibamiza Sevilla
-
Wagonga nyundo wa London washindwa kutamba mbele ya Spurs
-
Messi, Ronaldo, Neymar kuchuana mchezaji bora wa FIFA
Katika michezo mingine ya ligi kuu Romelu Lukaku aliisaidia Man Utd iliyokuwa ugenini kuibuka kidedea kwa bao 1-0 dhidi ya Southampton, huku Baye Niasse akifunga mabao mawili wakati Everton wakiiua Bournemouth 2 kwa 1.
Manchester City wameichapa Crystal Palace mabao 5-0 huku Raheem Sterling akifunga mara mbili mabo mengine yakifungwa na Leroy Sane, Kun Aguero na Fabian Delph.
Swansea City wakiwa nyumbani walifungwa mabao mawili kwa moja na Watford, mabao ya Watford yakifungwa na Andre Gray na Richarlison.