Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ameishauri Bodi ya Taifa na Wahasibu  na Wakaguzi wa hesabu (NBAA) kuwataja hadharani wahasibu wabadhirifu ili jamii iwajue.

Ametoa ushauri huo  Jijini Dar es salaam, wakati akizindua Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) kilichopo Bunju, aidha ametoa wito kwa wahasibu wote nchini kuisaidia Serikali  kupitia taaluma yao hasa kipindi hiki cha kuelekea Tanzania yenye uchumi wa viwanda ili kuharakisha maendeleo.

Aidha, Mpango amesisitiza umuhimu wa kukitunza kituo hicho ambacho Serikali itakitumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo mikutano ya Bodi ambayo imekuwa ikilipiwa gharama kubwa kwenye kumbi zingine.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mkuu wa NBAA, Pius Maneno amesema kuwa miaka 12 iliyopita walikuwa wakitumia  bilioni 1.5 kulipia kumbi hivyo kituo  hicho kitakuwa chanzo cha mapato.

Lema agonga mwamba tena
Serikali kumalizana na Dangote