Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina  ameutaka uongozi wa  Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS)  kuangalia na kupitia nyaraka walizonazo ili kuona uhalali wa umiliki wa eneo la hekta 20000 kwenye vitalu tisa vilivyopo kwenye Ranchi ya Uvinza inayomilikiwa na  Kampuni za Mifugo za Taifa (NARCO) kabla ya Selikali kuwatoa kwa nguvu ifikapo tarehe 1/1/2018.

Ametoa maelekezo  hayo alipotembelea ranchi ya Uvinza kuangalia shughuli mbalimbali ambapo ametoa muda wa hadi Januari mosi mwakani.

Aidha Mpina amesema endapo Mwekezaji huyo ataendelea kubaki  baada ya tarehe Mosi Januari, Serikali itamuondoa kwa nguvu na atatakiwa kulipa gharama zote za fidia na usumbufu.

“Ninakuagiza angalia taarifa mbalimbali ulizonazo kuhusu  umiliki wa eneo hili kama utaona umeendelea kukaa  hapa bila kufuata taratibu tafadhali uondoke mara mmoja ili kupisha Serikali kuendelea na shughuli zake,” amesema  Mpina

Hata hivyo, amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO, Prof  Philemoni Wambura  kuwaandikia  barua  ya kuwaondoa wawekezaji wote katika Ranchi hiyo ambao hawajaendeleza kwa zaidi ya asilimia 40  na kwamba wawekezaji ambao wamewekeza kwa zaidi ya asilimia arobaini wanatakiwa kukamilisha malipo yote kabla ya Januari mosi mwakani.

 

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 9, 2017
Kilimanjaro Stars yajiwinda dhidi ya Rwanda