Waziri wa Nishati, January Makamba ametembelea mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere ili kukagua na kuangalia hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 67.
Makamba aametembelea mradi huo Agosti 8, 2022 ambapo akiwa eneo la tukio amesema, “Mradi huu umeanza kujengwa Disemba 2018 kwa sasa tumefika asilimia 67, katika miaka miwili na nusu ya mwanzo (Kuanzia Disemba 2018 – June 2021) tulifikia asilimia 37.”
Waziri Makamba ameongeza kuwa, “Leo tuko asilimia 67 ni kasi kubwa katika kipindi hiki kifupi, sasa hivi hapa kazi inafanyika saa 24 hakuna mapumziko kwa hiyo kasi imeongezeka.”
Katika ziara hiyo ya kutembelea Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere, Waziri Makamba amembatana na Bodi ya Wakurugenzi Tanesco, Menejimenti ya Tanesco ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Maharage Chande na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari.