Kufuatia kitendo cha Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na mpinzani wake Raila Odinga kuombana msamaha hadharani kimewaibua wanasiasa wengi hasa hapa nchini Tanzania wakipongeza hatua iyo kubwa iliyofikiwa nchini Kenya.

Ambapo Rais Kenyatta aliungana na makamu wake, William Ruto kufanya maombi ya amani kwa taifa lao na kukutana na Kolonzo Musyoka ambao wote walisimama mbele ya hadhara kuombana radhi na kusameheana.

Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema amesema kitendo hicho ni cha kijasiri na kuwa  uchaguzi unapomalizika wananchi wanapaswa kupatana ili maisha yaendelee.

”Hapa nchini Rais Magufuli, Freeman Mbowe wanaweza kufanya hivyo mimi naona Lowassa amefungua njia ya majadiliano hayo kwa hatua yake ya kumtembelea Rais Ikulu. Pia nimefurahi kusikia kwamba Maalim Seif wakati alipomtembelea mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema yuko tayari kukutana na Rais, hatua hii ni mwelekeo chanya” amesema Mrema.

Viongozi wengine waliounga mkono kitendo hiko kilichofanyika nchini Kenya ni Mkurugenzi wa wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema aliyedai kuwa wanasiasa nchini wanapswa kuiga mfano huo wa Kenya na amesisitiza kuwa wapinzani wasichukuliwe kama maadui.

Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi (Chauma), Hashim Rungwe amepinga vikali yaliyofanyika Kenya kufanyika hapa nchini akidai kuwa utamaduni wa Kenya ni tofauti na utamaduni wa hapa nchini amesema kuwa Kenya ina watu wastaarabu katika demokrasia wakati Tanzania bado inajikongoja.

Nini maoni yako juu ya mitazamo tofauti ya wanasiasa juu ya kitendo kilichofanywa na waliokuwa wahasama enzi za uchaguzi wa urais nchini humo?.

Video: Makamba awapa neno viongozi wa dini kuhusu Mazingira
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Uswisi