Wakati wasanii karibia wengi hufikiria kuvaa viatu vya gharama kubwa ili waongeze muonekano wa ‘kistaa’, msanii wa maarufu wa mashairi ya ngano za mtindo wa kuongea, Mrisho Mpoto yeye anaamini hufaidika zaidi anapokuwa anatembea peku.

Mpoto ambaye huonekana akiwa peku hususan anapokuwa katika kazi zake za muziki, amesema kuwa faida kubwa anazopata ni pamoja na kuongeza uwezo wa kufikiria pamoja na kuongeza siku za kuishi.

“Ili uwe na akili lazima ukanyage chini. Ili uishi muda mrefu lazima ukanyage chini, unajua hili ni kosa la kiufundi ndio maana watu wanakufa haraka na ndio maana watu akili hawana kwa sababu mwi unakosa connection na udongo. Tunasema connection dot, kuna mahusiano makubwa kati ya ardhi na mwili wako. Ukuaji wako unategemea nature tuliyo nayo, maji tunayotumia, maji pamoja na udongo. Kwa hiyo kuna nguvu kubwa ambayo iko kwenye udongo,” Mpoto aliiambia Global TV.

Angalia Trailer ya mwisho ya Filamu Mpya ya James Bond ‘Spectre’
Fainali Ya CCM Na Chadema, Majiji Haya Yanahusika